Ghana: Polisi watakiwa kupunguza kujamiiana kuelekea uchaguzi mkuu

0
48

Kamanda wa Polisi jijini Accra, Afful Boakye-Yiadom amewataka maafisa wa polisi kuepuka kujamiiana wakati wakijiandaa kusimamia uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika takribani miezi mitatu ijayo.

Yiadom amewataka maafisa hao kula vizuri na kupunguza kujamiiana ili waweze kuwa imara na watekeleze majukumu yao kwa ufanisi.

“Jitunzeni, sote tunahitaji nguvu za kufanya kazi wakati wa uchaguzi. Nawashauri mle vizuri, mpunguze kiwango cha kujamiiana ili muwe na nguvu ya kufanya kazi kabla, wakati na baada ya uchaguzi,” amesema kamanda huyo.

Aidha, amewataka watumishi wa jeshi hilo kutoegemea upande wowote wa itikadi za kisiasa ili wafanye kazi yao kwa weledi bila upendeleo.

Ghana inatarajia kufanya uchaguzi mkuu Disemba 7 mwaka huu, ambapo Rais Nana Akufo-Addo anaamini kuwa atashinda kwa muhula wa pili.

Send this to a friend