Godbless Lema apewa hifadhi nchini Canada

0
63

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema ameelekea nchini Canada alikopewa hifadhi ya kisasa (political asylum).

Lema aliyekuwa nchini Kenya alikokimbilia akiwa na familia yake tangu Novemba 2020, ameondoka nchini humo Disemba 9, 2020 kwenda Canada, wakili wake George Luchiri Wajackoyah amethibitisha.

Lema ambaye alikamatwa muda mfupi baada ya kuingia Kenya akidaiwa kuwa hakuwa na nyaraka halali, alisema kuwa amekwenda nchini humo baada ya kutishiwa maisha nchini Tanzania. Hata hivyo, baada ya muda aliachiwa na kuendelea kubaki nchini Kenya.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alikwenda nchini Kenya kuonana na Lema kabla ya kuondoka.

Lema alishindwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020, ambapo alikuwa akigombea ubunge kwa muhula wa tatu, na nafasi hiyo kuchukuliwa na mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mrisho Gambo.

Send this to a friend