Gwajima: Machinga wanaorudi barabarani wanatumiwa na wafanyabiashara wakubwa

0
62

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Wanawake na Makundi Maalum, Dorothy Gwajima ametoa onyo kwa baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wanaowatumia wamachinga wadogo kuuza bidhaa zao ili kukwepa kodi.

Akizungumza katika mahojiano na ITV katika kipindi cha Dakika 45, Waziri amebainisha kuwa katika baadhi ya maeneo rafiki yaliyotengwa kwa ajili ya wamachinga, bado wameendelea kuona baadhi yao wakiondoka na kurudi barabarani, na baada ya kutafiti zaidi waligundua wanatumiwa na wafanyabiashara wakubwa kubeba biashara zao na kuuza bila utaratibu.

“Niwapelekee tu salamu, hawa ambao tumepata taaarifa zao tunaendelea na uchunguzi na tunasema hiyo siyo sawa tusijifiche kwenye migongo ya wamachinga na kuwashinikiza na kuwashawishi waende wakafanye biashara kwenye maeneo ambayo tulishasema siyo rasmi kwao.

Aidha Waziri Gwajima amewaomba wamachinga kuacha kutumiwa na wafanyabiashara hao na kuahidi kuwa mara Serikali itakapowapata watu hao sheria itafuata mkondo wake mara moja.

Send this to a friend