Hakimu adaiwa kumshambulia kwa kipigo mdeni wake baada ya kushindwa kumlipa TZS 35,000

0
73

Hakimu Mkazi kutoka Mahakama ya mwanzo ya Wilaya mkoani Mwanza, John Mugonya anadaiwa kumkamata na kumshambulia kwa kumpiga, Rhoda Charles (42) mkazi wa Nyegezi baada ya kushindwa kulipa deni la TZS 35,000 alizokuwa anadaiwa.

Kwa mujibu wa Raia Mwema, inadaiwa tukio hilo lilitokea Agosti 19, mwaka huu katika eneo la Mahakama hiyo baada ya Hakimu huyo kupata taarifa kwamba mdeni wake yuko ofisi jirani ya Chama cha Watu wenye Ulemavu Tanzania (CHAWATA).

Karani atakayepoteza kishkwambi kukatwa kwenye malipo yake

Anadai akiwa katika shughuli zake za ujasiriamali, Mugonya aliingia katika ofisi hiyo ili kuonana na mhudumu wa ofisi, na ndipo alipomuita na kumtaka aongozane naye mpaka ofisini kwake.

“Niliongozana naye ofisini kwake, tukiwa njiani karibu na ofisi akanishika shingoni akihoji kwa nini sijalipa pesa yake, na akinipigia simu sipokei, lakini kilichoniumiza zaidi akasema mimi ni tapeli. Aliponisukuma niliangukia kisogo, alipogundua niko chini, akakimbilia ndani akajifungia,” amedai.

Taarifa zinasema kwamba tayari Hakimu huyo amefunguliwa taarifa MW/RB/6110/2022 katika kituo kikuu cha polisi Nyamagana ambapo Rhoda alipewa fomu namba 3 na kutibiwa katika hospitali ya Mkoa ya Sekou Toure.

Chanzo: Raia Mwema.

Send this to a friend