Halima Mdee na wenzake waitwa kujieleza

0
25

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewataka wanachama wake 19 walioapishwa jana kuwa wabungr wa Viti Maalum kufika katika makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam Novemba 27, 2020 kujieleza juu ya kuapishwa kwao.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kusisitiza kuwa chama hicho hakijawasilisha majina na wabunge hao Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Mnyika ameongeza kuwa chama hakitambui uteuzi wa wabunge hao ambao waliapishwa Novemba 24, 2020 mbele ya Spika wa Bunge, Job Ndugai.

“Chama hakijawahi kuwasilisha majina yoyote wala kujaza fomu ya viti maalumu kuwakilisha chama hicho Bungeni”Amesema

Wabunge walioapishwa ni pamoja na aliyekuwa Mbunge wa Kawe Halima Mdee, aliyekuwa Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya na Esther Matiko ambaye alikuwa Mbunge wa Tarime Mjini.

Send this to a friend