Hamas yakubali kuwaachia mateka 50, Israel itawaachia Wapalestina 150

0
50

Viongozi wa mataifa mbalimbali wamepongeza uamuzi wa kundi la wanamgambo la Hamas kukubali kuwaachilia huru mateka walioshikiliwa tangu kuanza kwa mapigano Oktoba 7, mwaka huu.

Maafisa wa Israel na kundi la Hamas, walifikia makubaliano siku ya Jumanne juu ya usitishaji mapigano wa siku nne ili kuwezesha kundi hilo kuwaachia huru mateka 50 kati ya takribani watu 200 wanaoshikiliwa, hasa watoto na wanawake.

Taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Qatar iliyotolewa leo, imethibitisha kufikiwa kwa makubaliano hayo, ikisema wakati wa kuanza kusitishwa kwa muda mapigano utatangazwa katika muda wa saa 24.

Mmoja wa Watanzania wawili waliopotea nchini Israel afariki dunia

Kwa upande mwengine, Israel itawaachilia huru Wapalestina 150 wanoshikiliwa katika jela za Israel huku Hamas ikipongeza makubaliano hayo ya usitishaji wa muda kwa ajili ya kutekeleza zoezi hilo.

Waziri Mkuu, Benjamin Netanyahu amesema Israel itaanzisha tena vita baada ya mapatano hadi itakapofikia malengo ikiwa ni pamoja na kulishinda kundi la Hamas na kuwarejesha mateka wote.

Send this to a friend