Harmonize kutumbuiza jukwaani kwa siku tatu mfululizo

0
50

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize ametangaza kuandaa na kufanya tamasha la muziki katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ambapo atatumbuiza kwa siku tatu mfululizo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Harmonize amesema kuwa tamasha hilo ambalo amelipa jina la Harmo Night Carnival litaanza Novemba 28 mwaka huu.

Amesema katika tamasha hilo, wasanii mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi watatumbuiza, huku akiwataka wasanii wengine wanaotaka kutumbuiza kusema kiwango cha fedha wanachotaka kulipwa na muda watakaotumia jukwaani.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa kama ambavyo wasanii wengine wa kimataifa wanaweza kutumbuiza eneo moja hata kwa wiki nzima, basi hata hapa nyumbani itawezekana kwani kuna wasanii wenye vipaji.

Send this to a friend