Harmonize: Sijamdai Anjella hata senti moja

0
98

Mmiliki wa lebo ya Konde Music World Wide, Rajab Abdul maarufu Harmonize amefafanua kuwa hajamdai kiasi chochote cha pesa msanii wake Angelina Samson ‘Anjella’ licha ya maneno kusambaa mtandaoni kuwa amemdai hela.

Akiandika hayo kupitia mtandao wa Instagram, Harmonize amedai alikutana na msanii huyo akiwa ‘amejikatia tamaa’ na kuamua kumsaidia, na kuongeza kuwa endapo kuna mtu anayeweza kuendeleza kipaji cha binti huyo asisite kufanya hivyo.

“Nilikutana na Anjella akiwa amejikatia tamaa, akiwa na ndoto kichwani. Sikujiangalia nina kiasi gani, niliamini kwa kuwa watu wapo wananisupport bila kuwalipa senti 5 basi watasupport kipaji cha sister Anjella. Nilichoangalia ni ndoto hasa za mtoto wa kike,” ameandika.

Eng. Hersi akanusha kuwakashifu Yanga kuhusu ulaji mihogo

Ameongeza, “Nimejitahidi kadri ya uwezo wangu, najua kuna wenye uwezo mkubwa kunizidi ukizingatia nimeanza juzi, kama kuna anayeweza kumuendeleza kipaji chake ni faraja kwangu, asisite kujitokeza. Puuzia siasa za kusema sijui namdai mahela, never asked her even
1 cent,” ameandika Harmonize.

Anjella alitambulishwa rasmi kwenye lebo hiyo Machi 11, 2021 na kutoa nyimbo zilizofanya vizuri ikiwemo ‘Kama’ aliomshirikisha Harmonize, ‘Nobody’ na ‘Kioo’ ambazo zote zilipata watazamaji wengi katika mtandao wa Youtube.

Send this to a friend