Harmonize: Wasanii kuweni na nyimbo za Kiingereza

0
117

Msanii Rajabu Abdul maarufu ‘Harmonize’ amesema ni vizuri wasanii wa Afrika kuwa na nyimbo za Kiingereza katika orodha za nyimbo zao ili kuwafikia watu wengi duniani.

Akiandika kwenye ukurasa wake wa Instagram, Harmonize amepongeza jitihada zinazofanywa na wasanii wa Afrika ambapo sasa bara hilo linafanya vizuri katika burudani tofati na miaka ya nyuma, na kwamba ni wakati wa wasanii wa kiafrika kutotangulizwa kufungua shoo katika matamasha makubwa duniani.

“Najivunia soko la muziki wa Afrika, kuna wasanii ambao wanaweza kuimba Kiswahili, ambao wanaweza kuimba Kiingereza na wanaoweza kuimba vyote. Afrika Mashariki tunakuja kwa kasi, na kwa namna hii tunaweza kuacha ‘ku-perform’ shoo za mchana kwenye matamasha makubwa, kwa sababu tunawapa machaguo,” amesema.

Ameongeza, “wasanii wa Afrika msiache kuimba kwa lugha yenu, lakini hakikisheni mnaimba na nyimbo za Kiingereza ili kuendana na dunia,” ameeleza.