Hatma ya Mwijaku Mei 31 mwaka huu

0
81

Hukumu ya kesi inayomkabili msanii wa maigizo, Bulton Mwemba maarufu ‘Mwijaku’ inatarajiwa kutolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Mei 31 mwaka huu.

Mahakama chini ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rhoda Ngimilanga imefikia uamuzi huo jana baada ya Mwijaku na mashahidi wake wawili kumaliza kutoa utetezi wao.

Baada ya mahakama kusikiliza na kupitia ushahidi wa mashahidi watano wa upande wa Jamhuri na vielelezo vinne, mshtakiwa (Mwijaku) alikutwa na kesi ya kujibu.

Mwijaku anashtakiwa kwa kusambaza picha za ngono kupitia mtandao wa kijamii wa WhatsApp uliounganishwa kwenye kompyuta yake katika tarehe tofauti kati ya Septemba 17 na Oktoba 10, 2019 jijini Dar es salaam.

Send this to a friend