Hatua 6 za kufuata tairi likipata pancha barabarani

0
16

Ajali nyingi za barabarani ambazo kusababisha vifo au uharibifu hutokana na matairi yasiyo na sifa kwenye magari.

Kuna hatua mbalimbali za kufuata ndani ya dakika chache baada ya kupasuka kwa tairi ambazo unapaswa kuzifahamu.

1. Tulia
Usihamaki wala kukanyaga breki, tulia kwanza, kwa sababu mara baada ya kupasuka tairi, gari lako litaanza kwenda kombo na hivyo utahitajika kulimudu.

2. Shika usukani
Kamata usukani kwa nguvu kwa mikono yote miwili, usipinde kona huku ukiwa makini na barabara pamoja na vioo vya gari lako. Wakati huo soma mwenendo wa gari lako ambapo mara nyingi litakuwa linakuvuta upande uliopasuka tairi.

Mambo 6 yatakayobadilika baada ya kifo cha Malkia Elizabeth II

3. Ongeza mwendo
Ongeza mwendo wa wastani ili kudhibiti mwenendo wa gari. Hivyo kama ulikuwa umekanyanga eksileta usiondoe mguu haraka kwenye hiyo pedo.

4. Ondoa mguu kwenye eksileleta
Ondoa mguu wako taratibu kwenye eksileta. Usijaribu kabisa kukanyaga breki, ukijaribu kufanya hivyo utabinuka na gari.

Kama usipokanyaga breki gari litapunguza mwendo lenyewe taratibu, wakati wewe ukiwa makini kuangalia watumiaji wengine wa barabara.

5. Weka nyutro
Ondoa gia zote na uziweke kwenye nyutro huku bado ukiwa umeshikilia vyema usukani wako na macho mbele kwenye barabara.

6. Kanyaga breki
Baada ya muda mfupi kulingana na mwendo wako gari likiwa limefika spidi chini ya 60kph, sasa kanyaga breki zako taratibu huku ukisogea kando mwa barabara ili usimame, na hatimaye itakuwa salama kusimamisha gari lako na kuzima injini.