Hatua 6 za kuwarudisha wateja waliohama biashara yako

0
44

Sababu mbalimbali zinaweza kusababisha wateja kuhama na kuacha kutumia au kununua bidhaa zako. Kuwarudisha wateja hao inaweza kuwa mchakato mrefu kidogo, lakini kwa kuzingatia hatua mbalimbali inaweza kukurahisishia na kurejesha tena imani ya wateja wako wa zamani.

Kwa kufuata hatua hizi, unaweza kuwarudisha tena wateja waliohama na kujenga uaminifu na wateja wako;

Tafuta sababu za kuondoka
Ili kujua jinsi ya kuwarudisha, unahitaji kujua ni kwanini wateja hao wamehama. Sababu zinaweza kutofautiana kutokana na bei, ubora wa bidhaa au huduma. Fanya utafiti au wasiliana nao kujua kwanini walihamia kwa washindani au kuacha kutumia bidhaa yako.

Jenga uhusiano
Uhusiano bora na wateja ni muhimu. Wasiliana nao kwa njia ya kirafiki, na uonyeshe kujali mahitaji yao. Unaweza kuwasiliana nao kwa njia ya simu au barua pepe, ili kujenga uhusiano huo.

Toa motisha
Hii inaweza kujumuisha kupunguza bei, kutoa ofa maalum, punguzo, au zawadi kwa wateja wa zamani. Motisha hizi zinaweza kuwa njia nzuri ya kuwavuta kurudi.

Biashara 5 ambazo hupaswi kufanya ukiwa na mtaji mdogo

Boresha bidhaa au huduma zako
Kusikiliza mawazo na maoni ya wateja waliopita na kuboresha bidhaa au huduma zako kulingana na maoni hayo inaweza kuwavutia kurudi. Hakikisha pia unatoa huduma bora kwa wateja wako wa sasa ili na wao wasiondoke. Kutoa huduma nzuri kwa wateja zaidi ya mwanzo na kuongeza huduma za ziada kutaleta sifa nzuri, na hata wateja wako wa zamani watarudi wakisikia namna unavyohudumia.

Tangaza mabadiliko
Ikiwa umefanya mabadiliko au uboreshaji katika biashara yako, hakikisha unawasiliana na wateja wa zamani na kuwaarifu kuhusu mabadiliko hayo. Pia, unaweza kutumia mitandao ya kijamiii kutangaza maboresho ya huduma yako, kwa kufanya hivyo wanaweza kuwa na hamu ya kujaribu tena bidhaa au huduma zako mpya.

Endelea kufuatilia na kurekebisha
Baada ya kuanza kampeni ya kuwarudisha wateja, ni muhimu kufuatilia matokeo na kurekebisha mkakati wako kulingana na majibu ya wateja. Hii inaweza kujumuisha kuboresha motisha au kurekebisha zaidi huduma.

Send this to a friend