Hawa ndio wagombea 9 wanaowania Uspika wa Bunge la Tanzania

0
17

Saa chache ziliwa zimebaki kumfahamu atakayeongoza mhimili wa Bunge, Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi amesema wagombea tisa watawania naafasi hiyo katika uchaguzi utaofanyia Februari Mosi 2022.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma kuhusu uchaguzi huo na maandalizi ya uchaguzi Nenelwa amesema kuwa miongoni mwa Wagombea hao nane sio Wabunge na mmoja ni Mbunge.

Amewataja magombea hao kuwa ni;
1. Abdullah Mohammed Said (NRA)
2. Mhandisi Aivan Jackson Maganza (TLP)
3. David Daud Mwaijojele (CCK)
4. Georges Gabriel Bussungu (ADA -TEA),
5. Kunje Ngombale Mwiru (SAU),
6. Maimuna Said Kassim (ADC)
7. Ndonge Said Ndonge (AAFP)
8. Saidoun Abrahamani Khatib (DP) na
9. Dkt. Tulia Ackson (CCM)

Dkt. Tulia anapewa nafasi kubwa kushinda uchaguzi huo kutokana kwanza na uzoefu alioupata kwa miaka akiwa naibu spika, na chama chake kuwa na wabunge wengi.

Baada ya uchaguzi huo, mchuano utahamia kwenye kumpata Naibu Spika.

Send this to a friend