Baadhi ya watu kula chakula cha usiku muda usiofaa ni kawaida kwao kutokana na kuchelewa kurudi kutoka katika sehemu zao za kazi.
Sote tunajua kwamba ulaji usiofaa unaweza kuwa na madhara kwa afya yako. Lakini ni nini madhara ya kiafya kuchelewa kula wakati wa usiku?
Husababisha kitambi
Tafiti zinaonesha kuwa watu wanaochelewa kula usiku kwa kawaida hufanya uchaguzi mbaya wa chakula kwa kula vyakula vyenye kalori zaidi kama vile chipsi kutokana na wengine kukosa muda wa kupika vyakula, hivyo vinaweza kusababisha ukapata kitambi.
Husababisha mfumo wa chakula kuwa duni
Kula muda umeenda husababisha mfumo wa chakula kushindwa kufanya kazi yake vizuri. Usagaji ukiwa duni inaweza kukufanya uwe hatarini kupata magonjwa yasiyo ya lazima kama homa na mafua. Hii ni kwa sababu mwili wako hauwezi kusambaza virutubisho sahihi kwenye mwili.
Huathiri usingizi
Kula au kunywa chini ya saa moja kabla ya kulala kunaweza kusababisha hatari ya kukosa usingizi.
Unapokula usiku sana, misuli inayoyeyusha na kumetaboli chakula, lazima iendelee kufanya kazi muda unaopaswa kupumzika. Hii inaweza kukusababishia uchelewe kusinzia na inaweza kukuzuia kupata usingizi mzito.
Faida 7 za kufanya ‘meditation’ asubuhi
Husababisha kiungulia
Unapochelewa kula kisha ukaenda kulala kuna hatari ya kupata kiungulia kutokana na asidi ya tumbo huhama kwa njia isiyo sawa na kujilazimisha kurudi kwenye umio. Ili kuzuia hali hizi, kula chakula kidogo, lala baada ya masaa matatu na ikiwezekana kula matunda ikiwa utahisi njaa.