Haya ndio ‘Mazingaombwe’ yaliyofanyika ununuzi wa vishikwambi 300,000 vya Sensa

0
15

Ripoti iliyotolewa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2021/22 imebaini kasoro mbalimbali katika ununuzi wa vishikwambi 300,000 vyenye thamani ya TZS bilioni 123.78, kwa ajili ya Sensa ya Watu na Makazi mwezi Agosti, 2022.

Ripoti ya CAG imeeleza kasoro zilizojitokeza katika manunuzi hayo yaliyofanywa na Wizara ya Elimu ikiwa ni pamoja na kushindwa kuainisha bei za soko la vishikwambi, hivyo huenda vimenunuliwa kwa bei ya juu ikilinganishwa na bei ya soko.

Dosari nyingine ni kwamba bodi ya zabuni ilibadilisha vigezo vya ubora bila kuwasiliana na idara tumizi na kuondoa vifaa vya kutunzia umeme (power bank).

Orodha ya nchi 10 za Afrika zenye mamilionea wa dola wengi zaidi

Wizara ilitoa vishikwambi 209,480 kwa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) bila nyaraka sahihi au tarehe ya wazi ya makabidhiano na ripoti ya hali baada ya zoezi la sensa

Wazabuni walichaguliwa bila ushindani, pia wajumbe wa bodi ya zabuni walipendekeza wazabuni 4 kati ya 14, na wawili kati yao walishinda zabuni na kubainisha kuwa siyo kazi ya Bodi ya zabuni kupendekeza wazabuni.

Tofauti zilizopatikana kati ya bei za zabuni zinazojumuisha VAT katika taarifa ya ufunguzi wa zabuni na ripoti za tathmini ambapo zabuni hazikueleza hali ya VAT isipokuwa zabuni moja.

Hata hivyo imeeleza kuwa hakuna ushahidi wa hati ya udhamini uliotolewa kwa vishikwambi vilivyonunuliwa, kinyume na matakwa ya mkataba ulioainisha makubaliano ya hati ya miaka miwili.

Send this to a friend