Haya ni madhara ya kutumia simu wakati wa kulala

0
60

Daktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo, Uti wa Mgongo na Mishipa ya fahamu kutoka taasisi ya tiba na Mifupa (MOI), Lemery Mchone amesema matumizi ya simu na kompyuta mpakato kitandani ni chanzo cha kukosa usingizi hivyo watu wanapaswa kuepuka matumizi yasiyo muhimu kwa wakati huo.

Daktari amesema matumizi ya simu ni sababu ya mtu kutolala muda ambao ni sahihi kwani wengi hupitiwa kutokana na kuchati muda mrefu na kuathiri muda wa usingizi.

“Akili ya binadamu inatakiwa kupumzishwa saa nane kwa siku ili kuwa na uwezo wa kuimarisha afya ya akili ya kila mtu, hivyo kitendo cha kutumia muda wa usingizi kufanya vitu ambavyo havina ulazima kunaathiri afya hiyo,” amesema.

Serikali kuwachukulia hatua wote waliohusika tukio la watu wa jinsia moja kuvalishana pete 

Aidha, Chuo cha Royal of Paediatrics (RCPCH) kinachosimamia mafunzo ya wataalam wa dawa za watoto, umebaini kuwa matumizi ya simu muda wa kulala huathiri saa ya kibaiolojia. Kutumia simu ya mkononi, kompyuta au kifaa kingine cha kielektroniki kinachotoa mwanga kwa zaidi ya saa moja kitandani, kinaweza kupunguza uzalishaji wa melatonin inayohusika na utengenezaji wa usingizi.

Pamoja na hayo, wamebainisha kuwa husababisha maumivu ya misuli ya macho na mwili kwa ujumla, hususani ni misuli ya shingo inayojulikana kitaalam kama sternocleidomastoid, hivyo humfanya mtu kuwa na maumivu ya muda mrefu ya shingo.

Send this to a friend