Heche na wenzake washinda shauri la kuidharau Mahakama

0
54

Mahakama Kuu Dar es Salaam imetupilia mbali shauri la maombi ya kuidharau Mahakama iliyofunguliwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Saidi Issa na wenzake dhidi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche na wenzake.

Wajibu maombi wengine katika shauri hilo la madai ya kudharau amri ya mahakama hiyo ni Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, Rose Mayemba, Brenda Rupia, Hilda Newton, Twaha Mwaipaya Gervas Bernard Lyenda, na wadhamini waliosajiliwa wa CHADEMA.

Viongozi hao walidaiwa kukiuka amri ya kukizuia chama hicho kufanya shughuli za kisiasa na kutumia mali za chama hicho hadi hapo kesi ya mgogoro wa mgawanyo wa rasilimali baina ya CHADEMA Bara na CHADEMA Zanzibar itakapoamuliwa.

Hata hivyo, Mahakama chini ya Jaji Awamu Mbagwa imekubaliana na pingamizi lililokuwa limewekwa na Wakili wa utetezi, Hekima Mwasipu kuwa maombi hayo yameletwa mahakamani hapo nje ya muda wa siku 60.

Send this to a friend