Hii ndio mikoa 15 ya kwanza aliyounda Mwl. Nyerere baada ya uhuru

0
80

Wakati Tanganyika, sasa Tanzania Bara, inapata uhuru kutoka kwa Uingereza mwaka 1961, Mwalimu Julius Nyerere alipokea nchi ikiwa katika mfumo wa majimbo, ambapo kulikuwa na majimbo nane, na sio mikoa kama ilivyo sasa.

Majimbo hayo ni Jimbo la Kati, Jimbo la Mashariki, Jimbo la Ziwa, Jimbo la Kaskazini, Jimbo la Nyanda za Juu Kusini, Jimbo la Tanga, Jimbo la Magharibi na Jimbo la Ziwa Tanganyika.

Kwa mamlaka aliyopewa na katiba ya nchi, Mwalimu Julius Nyerere aliunda mikoa 15 na kuiondoa nchi katika utaratibu wa majimbo.

Mikoa hiyo ni Arusha, Pwani, Dodoma, Tanga, Kigoma, Kilimanjaro, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Ruvuma, Shinyanga, Singida na Tabora.

Hadi mwaka 2021 mikoa hiyo imeongezeka na kufikia 26 huku halmashauri zote (wilaya, miji, manispaa, majiji) zimeongezeka kutoka 45 wakati wa uhuru hadi 184, lengo likiwa ni kusogeza madaraka kwa wananchi na kuimarisha utoaji wa huduma za kijamii.

Mwaka 1972 serikali ilifuta Mamlaka za Serikali za Mitaa na kuanzisha mfumo wa madaraka mikoani, mfumo ambao ulizifanya serikali za mitaa kuitegemea serikali kuu kwa kila jambo kutokana na wananchi kutoshiriki katika maamuzi na pia katika shughuli za maendeleo.

Miaka sita baadaye, mamlaka za miji zilirejeshwa huku mamlaka za wilaya zikirejeshwa mwaka 1984.

Katika moja ya mahojiano aliyowahi kufanya enzi za uhai wake, Mwl. Nyerere alikiri na kusema anajutia kufuta mamlaka za serikali za mitaa.

Send this to a friend