Hii ni sababu kwanini hutakiwi kuoga wakati kuna radi

0
35

Palipo na radi kuna umeme, na umeme unaweza kuua au kulemaza kwa njia zisizotarajiwa. Hivyo inajumuisha unapooga, kufua kwenye beseni au hata kuosha vyombo.

Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa Marekani (CDC) kimesema umeme unaweza kusafiri kupitia mabomba hivyo ni bora kuepuka matumizi yoyote ya maji wakati wa radi ikiwa ni pamoja na kuoga, kuosha vyombo, kunawa mikono au hata kushika mabomba ya maji.

“Hatari ya umeme kusafiri kupitia mabomba inaweza kuwa ndogo kupitia mabomba ya plastiki kuliko mabomba ya chuma. Hata hivyo, ni vyema kuepuka kugusa mabomba na maji wakati wa radi ili kupunguza hatari yako ya kupigwa,” imesema CDC.

Imeshauri pia watu kuepuka kukaa karibu na madirisha, milango au kulala kwenye sakafu pamoja na kuepuka matumizi ya vitu vyovyote vilivyounganishwa kwenye umeme kama vile kompyuta au vifaa vya kielektroniki, na kuepuka matumizi ya simu za waya kwani simu zisizo na waya ni salama ikiwa hazijaunganishwa kwenye umeme kupitia chaja.

Fanya mambo haya 13 kama uko kwenye miaka ya 20+

CDC inasema vifo vingi na majeraha hutokea wakati watu wako nje, haswa wakati wa miezi ya kiangazi mchana na jioni, hivyo ni vyema kukaa eneo salama ili kujikinga.

“Ukikutwa nje, usilale chini. Radi husababisha mikondo ya umeme juu ya ardhi ambayo inaweza kuwa hatari zaidi. Ingia ndani ya eneo salama, nje si sehemu salama,” imeeleza taarifa yao.

Send this to a friend