Harakati za Siku ya Wanawake Duniani zilianza mnamo mwaka 1908 ambapo jumla ya wanawake 15,000 waliandamana katika Mji wa New York wakidai kupunguziwa muda wa kufanya kazi, kupata ujira wa kuridhisha na kupewa haki ya kupiga kura.
Mwaka 1909 mwanamke mmoja mwanaharakati wa kikomunisti na mtetezi wa haki za wanawake, Clara Zetkin alipendekeza kuanzishwa kwa Siku ya Wanawake Duniani ambayo haikuwa na tarehe maalum katika mkutano wa wafanyakazi wanawake uliofanyika jijini Copenhagen nchini Denmark.
Hata hivyo haikurasimishwa hadi tarehe ambapo mgomo wa wanawake ulianza Jumapili tarehe 23 Februari kwa kalenda ya Julian ambayo wakati huo ilikuwa ikitumika nchini Urusi. Siku hii katika kalenda ya Gregori ilikuwa tarehe 8 Machi ambayo ndiyo tarehe inayoadhimishwa.
Kwa mara ya kwanza siku hii ilisherehekewa mwaka 1911 ambapo mataifa 11 yalikusanya wanawake mia moja kuiadhimisha. Tarehe 8 Machi 1975 siku hii ilianza kuadhimishwa duniani kote baada ya Umoja wa Mataifa (UN) kuridhia siku hii kutumika kama siku rasmi ya kuikumbusha dunia juu ya haki za wanawake.