Historia fupi ya maisha ya Mwendazake Rais Mstaafu Benjamin Mkapa

0
61

Benjamin William Mkapa alikuwa mwanasiasa wa Tanzania ambaye alikuwa Rais wa Awamu ya Tatu kuanzia mwaka 1995 ulipofanyika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi hadi mwaka 2005. Katika kipind hicho alikuwa pia Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Mzee Mkapa amefariki dunia Julai 23, 2020 hospitalini jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu akiwa na umri wa miaka 82.

Alizaliwa mwaka 1938 huko Ndanda mkoani Mtwara ambapo alianza kupata elimu huko na alihitimu Shahada ya Lugha ya Kiingereza katika Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda mwaka 1962. Alijiunga na Chuo Kikuu cha Columba na kuhitimu Shahada ya Umahiri katika kada ya uhusiano wa kimataifa.

Enzi za uhai wake alishika nyadhifa mbalimbali serikali na ndani ya chama ikiwa ni pamoja Waziri wa Elimu, Afisa Tawala wa Dodoma, Balozi wa Tanzania nchini Canada, Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Mhariri Mkuu wa Gazeti la Serikali “The Nationalist” na Mwandishi wa Rais wa Kwanza wa Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Akiwa madaraka kama Rais wa Tanzania alifanya mapinduzi makubwa ya kiuchumi na kuruhusu uchumi wa soko huria.

Mzee Mkapa alifanikisha kuunda mamlaka na mashirika/taasisi mbalimbali za serikali zikiwemo Mamlaka za Serikali kama Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Wakala Barabara Tanzania (TANROADS), taasisi na mifuko ya kuinua wananchi kama MKUKUTA, MKURABITA pamoja na taasisi za udhibiti.

Rais Mkapa ameacha mke na watoto wawili.

Send this to a friend