HIVI PUNDE: Rais Samia Suluhu afanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri kama ifuatavyo:
- George Boniface Simbachawene, Waziri wa Katiba na Sheria, amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera na Uratibu.
- Damas Daniel Ndumbaro, Waziri wa Maliasili na Utalii amehamishiwa Wizara ya Katiba na Sheria kuwa Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria.
- Pindi Hazara Chana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge, Sera na Uratibu) amehamishiwa Wizara ya Maliasili na Utalii kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.