Hizi ndizo fani 6 zitakazopewa mikopo kwa wanafunzi wa Diploma

0
24

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema wanafunzi takribani 8000 watakaodailiwa kusoma stashahada katika fani zitakazopewa kipaumbele, watakaribishwa kuomba mikopo yenye thamani ya TZS bilioni 48 inayotolewa na ufadhili wa Samia Scholarship.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam, Waziri Mkenda amesema mikopo itakayotolewa ni kwa wanafaunzi wanaosoma fani ambazo zinahitajika zaidi nchini ambazo pia fani hizo zimeainishwa katika maeneo yaliyopewa kipaumbele.

Waziri Mkenda ametaja fani hizo kuwa ni afya na sayansi shirikishi, ualimu (fizikia, hisabati na mafunzo ya amali), usafiri na usafirishaji, uhandisi na nishati, madini na sayansi ya ardhi na kilimo na mifugo.

“Sio kila anayesomea stashahada ya ualimu atanufaika [kupata mkopo]. Humu tumeainisha maeneo ambayo tunapata shida sana kupata walimu […] Lakini tumeongeza mafunzo ya amali kwa ajili kuandaa walimu watakaotusaidia katika mkondo wa sekondari wa amali,” amesema.

Polisi Kenya wapewa ruhusa ya kuua majambazi wanaowashambulia

Aidha, amesema Serikali inafanya mkakati wa kuanzisha mfuko ambao utapanua Samia Scholarship ili kuwezesha wanafunzi kusoma katika maeneo mengine ikiwa ni pamoja na wale wanaoenda kufanya masters au PhD katika maeneo muhimu.

Uamuzi huu wa kutoa mikopo kwa wanafunzi wa stashahada, unatokana na marekebisho ya Sheria ya Bodi ya Mikopo mwaka 2017.

Send this to a friend