Hizi ndizo ndege zote zilizonunuliwa na serikali tangu 2016
Serikali ya Tanzania leo inapokea ndege mbili mpya aina ya Airbus 220-300 ambazo zitafanya jumla ya ndege zilizonunuliwa tangu mwaka 206 kufikia 11.
Ndege hizo zimenunuliwa na kukodishwa kwa Kampuni ya Ndege Tanzania kwa lengo la kufufua shirika hilo ili kukuza sekta ya utalii, kutoa ajiri na kujenga hadhi na heshima ya Taifa.
Hapa chini ni taarifa ya ndege zote ambazo zimenunuliwa na serikali.
1. Ndege mbili aina ya Bombardier Dash 8 – Q400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja ambazo ziliwasili nchini Septemba 2016 na kuanza kazi Oktoba 2016.
2. Ndege moja aina ya Bombardier Dash 8 – Q400 iliyowasili nchini Aprili, 2018.
3. Ndege moja ya masafa marefu aina ya Boeing 787 Dreamliner yenye uwezo wa kubeba abiria 262 ambayo iliwasili nchini Julai 2018.
4. Ndege mbili aina ya Airbus 220 – 300 zenye uwezo wa kubeba abiria 127 kila moja ambapo moja iliwasili nchini Desemba 2018 na nyingine iliwasili Januari 2019.
5. Ndege Boeing 787-8 Dreamliner yenye uwezo wa kubeba abiria 262 iliyowasili nchini Oktoba 2019
6. Ndege moja aina ya Bombardier Dash 8 – Q400
7. Ndege moja aina ya Dash 8 Q400 iliyopokelewa nchini Julai 2021
8. Ndege mbili aina ya Airbus A220-300 zinazopokelewa leo Oktoba 8, 2021.