Hizi ni athari za kutumia dawa za kuondoa kitambi

0
78

Vitambi ni tatizo linalowatesa watu wengi katika karne hii, jitihada nyingi za kuondoa tatizo hili zimekuwa zikifanyika ikiwemo kutumia dawa ya asili ya kuondoa vitambi. Lakini dawa hizi ni salama kwa afya?

Kwa mujibu wa Daktari Victoria Msambichaka kutoka Kampuni ya Vpreatta Group Limited, anasema dawa za asili zinazotumika kupunguza kitambi zinaweza kusababisha hatari pale mtu anapozidisha kipimo au akapunguza, na kutengeneza magonjwa mengine.

Anasema mtumiaji hajui anachokiingiza kwenye mwili wake kama kitakwenda kuathiri mifumo ndani ya mwili.

Aina 6 ya vyakula vya kuepuka unapotumia dawa

“Dawa zinakwenda kuathiri mfumo wa homoni, homoni ikipata hitilafu mfumo wa mwili hubadilika, ndipo unasikia mtu anapata maumivu makali wakati wa hedhi, na wakati mwingine kupata ujauzito ni shida,” amesema Dk. Msambichaka.

Ameongeza kuwa zipo aina ya dawa ambazo humsaidia mtu kupunguza kitambi, lakini baada ya muda fulani hupata kitambi kikubwa zaidi.

“Kwa watumiaji wa dawa za hospitali au kienyeji wengi huharisha sana, hatari iliyopo mtu hupoteza madini muhimu mwilini. Madini haya yakiondoka mwilini mtu anapungua lakini hana afya, tofauti na wale wanaopungua halafu wana afya,” ameeleza Dk. Msambichaka.

Chanzo: Mwananchi