Hizi ni faida 5 za kula bamia

0
34

Ulaji wa bamia umekuwa ukikimbiwa na watu wengi licha ya kutajwa kuwa msaada mkubwa katika mwili wa binadamu.

Kwa mujibu wa tovuti ya afya ya Healthline, hizi ni faida tano kubwa za ulaji wa bamia katika mwili wako.

Hupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo
Viwango vya juu vya cholesterol vinahusishwa na hatari kubwa ya ugonjwa wa moyo. Utafiti mmoja uliojumuisha kati ya watu 1,100 ulionesha kuwa wale waliokula bamia kwa wingi walikuwa na uwezekano mdogo wa kupata ugonjwa wa moyo.

Kuzuia saratani
Bamia ina aina ya protini inayoitwa ‘lectin’ ambayo inaweza kuzuia ukuaji wa seli za saratani ya binadamu. Utafiti mmoja katika seli za saratani ya matiti uligundua kuwa lectin katika bamia inaweza kuzuia ukuaji wa seli za saratani kwa hadi asilimia 63.

Inaweza kupunguza sukari kwenye damu
Kuongezeka kwa sukari kwenye damu kunaweza kusababisha ugonjwa wa kisukari. Watafiti walipendekeza kuwa bamia inasaidia ufyonzaji wa sukari kwenye njia ya kumeng’enya chakula, na hivyo kusababisha mwitikio thabiti zaidi wa sukari kwenye damu.

Huwasaidia wanawake wajawazito
Folate (vitamini B9) ni kirutubisho muhimu kwa wanawake wajawazito. Husaidia kupunguza hatari kwenye mirija ya neva ambayo huathiri ubongo na mgongo wa kijusi kinachokua.

Bamia ni chanzo kizuri cha folate, na kikombe 1 (gramu 100) hutoa asilimia 15 ya mahitaji ya kila siku ya mwanamke mjamzito.

Ina wingi wa virutubisho
Bamia ni chanzo bora cha vitamini C na K1. Vitamini C ni kirutubisho ambacho huchangia utendakazi wako wa kinga kwa ujumla. Pia ina Magnesiamu, protini, wanga, vitamini A, vitamini C, wanga n.k ambavyo ni muhimu kwenye mwili wako.

Send this to a friend