Hospitali ya Bugando yaanza utafiti kuhusu maji ya maiti kutumika kuhifadhia samaki

0
39

Kufuatia agizo la Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango kutaka kufanyike utafiti kuhusu kinachodaiwa kuwapo ongezeko la saratani mikoa ya Kanda ya Ziwa linalosababishwa na maji ya kuhifadhia maiti kutumika kuhifadhi samaki, hospitali ya Rufani ya Kanda ya Bugando imeanza utafiti wa kisayansi.

Utafiti huo unafanyika kupitia sampuli mbalimbali za wagonjwa wa saratani pamoja na wale wasiokuwa na ugonjwa huo wanaoishi Kanda ya Ziwa ili kubaini ukweli wa madai hayo.

Hayo yamebainishwa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani na Mkuu wa Idara ya Saratani hospitalini hapo, Dkt. Nestory Masalu wakati wa maadhimisho ya Siku ya Saratani Duniani ambaye ameeleza kuwa utafiti huo unatarajiwa kuchukua muda wa miezi sita.

Vijana milioni 1.7 Tanzania hawana ajira

“Tayari tumekusanya sampuli 7,000 za watu wenye saratani mbalimbali pamoja na sampuli 7,000 za watu wasiokuwa na saratani, wote wakiwa na umri ule ule na wanaishi mazingira hayo hayo ili tujue sababu za hawa kupata ugonjwa huo na wengine kutokupata ugonjwa huo,” ameeleza

Dkt. Masalu amesema majibu ya utafiti huo unatarajiwa kutolewa baada ya miezi sita kutokana na ugonjwa huo kuchukua muda mrefu kuleta majibu sahihi.

Kwa mujibu wa Dkt. Masalu wagonjwa wanaopokelewa hospitalini hapo wenye magonjwa ya saratani ni takribani wagonjwa 1500 kwa mwaka idadi inayoonekana kuwa kubwa zaidi.

Send this to a friend