Hoteli 5 kongwe zaidi Afrika na gharama zake kwa usiku mmoja

0
19

Kwa mujibu wa Business Insider Africa imetoa orodha ya hoteli kongwe zaidi barani Afrika huku baadhi ya hoteli hizo zikipokea wageni kwa takribani miaka 200.

Hizi ni Hoteli kongwe zaidi barani Afrika pamoja na bei zake kwa usiku mmoja;

1. Hoteli ya Houw Hoek, Afrika Kusini
Hoteli hii imekuwepo tangu mwaka 1779 katikati mwa Hifadhi ya Mazingira ya Kogelberg nchini Afrika Kusini. Iko umbali wa kilomita 80 kutoka Cape Town.

Unaweza kufurahia historia nzuri kwa $100 (sawa na TZS 233,200) kwa usiku, kulingana na Booking.com.

2. Hoteli ya Continental, Morocco
Iko Tangier nchini Morocco. Ilianzishwa mwaka 1870. Usanifu wa mapambo ya kale na miti ya tende ambayo wageni hupata kufurahia ni baadhi vitu vinavyopendwa zaidi. Wageni wanaweza kufurahia wifi ya bure na kifungua kinywa bila malipo, huku bei kwa kila chumba ikianzia $48 (sawa na TZS 111,936).

Nchi 10 duniani zinazoongoza kuwalipa walimu mishahara mikubwa

3. Marriot Mena House , Misri
Ilianzishwa mwaka 1886, ni hoteli ya kifahari ya nyota 5 huko Cairo, Misri. Kama ilivyo kwa Continental hotel, hoteli hii ya zamani pia ina mandhari nzuri ya kiafrika, bwawa la kuogelea la nje, mgahawa, kituo cha mazoezi ya mwili, spa na baadhi ya huduma.

Unaweza kufurahia anasa zote kwa $282 (sawa na 657,624) kwa usiku mmoja.

4. Hoteli ya El Djazair, Algeria
Hoteli hii ya kihistoria ilianzishwa huko Algiers mnamo 1889, imekadiriwa kuwa hoteli ya nyota 5, na vyumba vyake vya kigeni vinagharimu takriban $174 (sawa na 405,768) kwa usiku. Inatoa huduma za masaji, matibabu ya mwili, uwanja wa tenisi wa nje, kilabu cha usiku, sauna n.k.

5. Hoteli ya Grand Holiday Villa, Sudan
Hoteli hii imekuwepo tangu 1890. Inapatikana Khartoum, Mji mkuu wa Sudan na inatoa huduma mbalimbali kama gym, sauna, vifaa vya mikutano, kituo cha biashara, kunyoa n.k.

Vyumba katika hoteli hii viko katika makundi tofauti na kwa bei tofauti ambapo hufikia hadi $272 (sawa na TZS 634,304) kwa usiku.

Ukipewa nafasi, ungependelea kutembelea ipi kati ya hizi?