‘House boy’ kortini kwa tuhuma za shambulio la aibu kwa mtoto

0
103

Fred Kelendo Marekioli (19) mfanyakazi wa ndani (House boy) na mkazi wa Nyakato mkoani Mwanza, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Nyamagana mkoani humo kwa tuhuma za kumfanyia shambulio la aibu mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 5.

Wakili wa Serikali, Tunu Msangi ameieleza mahakama hiyo kuwa tukio hilo lilitokea Septemba 9, 2025 katika eneo la Mwananchi jijini humo, ambapo mshtakiwa anadaiwa kutenda kitendo hicho cha ukatili dhidi ya mtoto huyo.

Hata hivyo, mshtakiwa amekana shtaka hilo. Hakimu Ramla Shehagilo anayesikiliza kesi hiyo ameeleza kuwa kosa hilo linadhaminika kwa masharti, ikiwemo kuwa na wadhamini wawili wenye vitambulisho halali vya taifa, barua za utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa na kila mdhamini kusaini hati ya dhamana ya Shilingi milioni 1.

Mshtakiwa ameshindwa kukidhi masharti ya dhamana jambo lililosababisha kurudishwa rumande hadi Septemba 23, 2025, kesi hiyo itakapoitwa kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa hoja za awali.

Send this to a friend