Huduma ya pesa kwa njia ya simu inavyoweza kutusaidia kupunguza maambuki ya corona

0
22

Homa ya corona imetikisa kila kona ya dunia hivi sasa. Tanzania nako si kisiwa kwani napo visa vya maambukizi vilianza kupatikana kuanzia mwezi Machi. 

Katika nyakati za changamoto hii ni lazima kuhakikisha sote tunashirikiana ili kuzuia kuenea kwa maambukizi ya kirusi cha homa hii. 

Tumeona namna watu binafsi na hata wafanyabiashara wanavyobuni mbinu mpya ili maisha yaweza kuendelea huku tukipambana kuzuia maambukizi. Sekta ya usafiri ilikuwa moja ya sekta za mwanzo sana kutafuta mbinu mbadala kuendelea na biashara, kwa mfano Dar es Salaam serikali ilisema lazima daladala zote watu wawe wameketi, mkoani Ruvuma wao wakasema nauli za mabasi watalipana kwa njia ya simu jambo ambalo lilipunguza msongamano wa kufanya malipo vituoni. 

Shirika la Afya Duniani (WHO) nalo likasisitiza kwamba kufanya malipo kwa njia za kielektroniki kama simu au kadi inasadia kupunguza maambukizi kwa kuondoa uwezakano watu kugusana mikono na kukutana ana kwa ana.  

Bahati nzuri miaka ya karibuni Watanzania wengi wanatumia mitandao ya simu kwa huduma za kifedha hasa kutuma na kupokea hivyo basi kulipia huduma kwa njia ya simu haijawa jambo gumu kuzoea na kuendelea nalo.  

Mbali na kusaidia kupunguza maambukizi, fedha kwa njia ya simu imesaidia kuwaleta watu wengi zaidi kwenye mfumo rasmi wa kifedha hasa walio vijijini. Imepunguza athari za kutembea na mzigo wa fedha pia na imejenga ajira za wale wenye vibanda vya fedha. 

Huduma hizi za fedha kwa njia ya simu ni za kibunifu katika teknolojia na zimewezekana kutokana na kazi kazi kubwa ya kampuni za mawasiliano ya simu kama Tigo Tanzania. Tigo inajipambanua kama kampuni inayoa huduma mbalimbali za kifedha kupitia programu elekezi yake (app) na kawaida na kusaidia mamilioni ya Watanzania kulipa kwa njia ya simu na kuendelea na maisha huku wakijikinga na maambukizi ya corona. 

Katika nyakati hizi, inatia faraja kuona tuna ubunifu kama huu wa kiteknolojia unaoweza kuchangia kwa kiasi fulani kupunguza maambukizi ya gonjwa hili hatari na kutuweka salama. 

Send this to a friend