Hungary yatangaza kufungua tena ofisi zake Tanzania

0
25

Serikali ya Hungary imetangaza dhamira ya kufungua tena Ubalozi wake hapa nchini tangu ilipoufunga mwaka 2000 ili kufungua ukurasa mpya wa ushirikiano baina yake na Tanzania kwa maslahi mapana ya nchi hizo mbili.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Hungary, Peter Szijjártó wakati wa mazungumzo rasmi na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiririano wa Afrika Mashariki,, January Makamba (Mb.) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.

Tanzania na Hungary kwa muda mrefu zimekuwa zikishirikiana katika maeneo ya biashara, elimu, uwekezaji na utalii huku zikiweka mikakati ya kupanua wigo wa ushirikiano.

Aidha, nchi hizo mbili zimesaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Sekta ya Maji huku zikiazimia kuongeza ushirikiano kwenye biashara, kushirikiana katika kujenga kiwanda cha kutengeneza ndege ndogo mkoani Morogoro ambapo zinaangazia kusaini Mkataba wa Usafiri wa Anga.

Kwa upande wa Tanzania, inatarajia kufungua Konseli Kuu ama Konseli ya Heshima jijini Budapest, zote zikiwa ni jitihada za kukuza ushirikiano wa Tanzania na Hungary.

Szijjártó yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ikiwa ni ziara ya kwanza ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Hungary tangu ziara ya mwisho mwaka 1987.

Send this to a friend