Huyu ndiye Kanali Mstaafu, Abdulrahman Kinana

0
65

Mwanasiasa aliyezaliwa mwaka 1952 mkoani Arusha, Baba yake, Mzee Omary Kinana alihamia Tanzania akitokea Somalia alipokuwa mtoto, anatokea katika ukoo wa kisomali wa Sheekhaal.

Alihitimu shahada yake katika Chuo Kikuu cha Harvard nchini Marekani. Pia aliwahi kuwa Spika wa Bunge la Afrika Mashariki mwaka 2001 mpaka mwaka 2006.

Kinana alishika nyadhifa mbalimballi Serikalini zikiwemo Waziri wa Ulinzi na Naibu Waziri wa Wizara ya mambo ya nje.

Aliwahi kutumikia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa muda wa miaka 20 kabla ya kustaafu kama Kanali mwaka 1992.

Pia aliwahi kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM jimbo la Arusha kwa muda wa miaka 10.

Kinana ana mchango mkubwa katika Chama cha Mapinduzi na anakumbukwa zaidi alipokuwa Katibu Mkuu na namna alivyoshirikiana na viongozi wengine kukiimarisha.

Ziara za Kinana ziliinua uhai wa CCM nchi nzima na kuongeza kasi ya utekelezaji wa ilani kwa kutatua kero za wananchi katika maeneo yao, kiasi cha kuongeza imani ya wananchi kwa CCM tofauti na ilivyokuwa awali.

“Nimepata barua ya Kinana ya kujiuzulu nafasi yake pamoja na wakuu wa idara za sekretarieti. Nimeamua Kinana na sekretarieti yote waendelee kuwepo.” hayo ni maneno ya Hayati John Magufuli baada ya kupokea barua ya Kinana ya kuachia nafasi yake ya Ukatibu Mkuu ambapo alikataa shauri lake la kujiuzulu nafasi hiyo na kumtaka aendelee mwaka 2017.

Kinana alichukuwa nafasi ya Katibu Mkuu CCM kutoka kwa Wilson Mukama mwaka 2012 na aliiachia nafasi hiyo mwaka 2018 ambapo nafasi hiyo ilichukuliwa na Dk Bashiru Ally.

Machi 31, 2022 chama hicho kimempitisha kuwa Makamu Mwenyekiti baada ya Philip Mangula, aliyekuwa akishika wadhifa huo, kutangaza kustaafu kwa hiari.

Send this to a friend