ICC yatoa hati ya kukamatwa Rais Vladimir Putin

0
40

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imetoa hati ya kukamatwa kwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin kwa uhalifu wa kivita ikiwa ni pamoja na kuwahamisha watoto kutoka Ukraine kwenda Urusi kinyume cha sheria.

Katika taarifa yake, mahakama imesema Putin alifanya uhalifu huo katika kipindi cha kuanzia Februari 24, 2022 wakati Urusi ilipoanzisha uvamizi wake rasmi nchini Ukraine.

Pia mahakama imetoa kibali cha kukamatwa kwa Maria Alekseevna Lvova-Belova, Kamishna wa Haki za Watoto katika Ofisi ya Rais wa Shirikisho la Urusi kwa madai sawa na hayo.

Mtoto wa Rais Yoweri Museveni atangaza kugombea Urais 2026

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi, Maria Zakharova amesema hati za kukamatwa hazina maana yoyote.

Moscow imekanusha madai kuwa wanajeshi wake wametekeleza vitendo vya kihalifu wakati wote wa vita.

Send this to a friend