Idadi ya wagonjwa wa figo Muhimbili yazidi kuongezeka

0
61

Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa Mohamed Janabi amezungumza kuhusu ongezeko la wagonjwa wa kusafisha figo ambapo amesema kwa siku hospitali hiyo inahudumia wagonjwa 120 hadi 130, hivyo ameihimiza jamii kuchukua tahadhari na kufuata mtindo bora wa maisha.

Profesa Janabi amesisitiza kwamba vitu hatari zaidi kwa afya ya mwili ni sukari na wanga na wala sio mafuta kama wengi ambavyo hudhani, na kwamba mwili hautunzi wanga wala sukari, badala yake huvibadilisha kuwa mafuta. Hivyo, amewataka watu kupunguza matumizi ya vyakula vyenye sukari na wanga.

Watumishi wa afya wasimamishwa kazi kwa kutofanya usafi

“Sukari ni ugonjwa hausababishwi na fangasi, hausababishwi na bacteria, unasababishwa na lishe, lazima tubadilishe mtindo wa maisha, mtakaopata nafasi mzungumze na mtu anayefanyiwa dialysis (kusafisha figo) ndio mtafahamu umuhimu wa kutunza figo,”amesema.

Profesa Janabi ameeleza kuwa kuepuka ugonjwa huo ni jambo linalowezekana kwa kubana matumizi ya chakula, kutembea kwa hatua 10,000 kwa siku, na kupunguza vyakula vyenye sukari. “Bei ya sukari imepanda juu, take advantage.”

Send this to a friend