Idadi ya watia nia wa CCM katika mikoa mbalimbali ya Tanzania

0
63

Wakati zoezi la kuchukua fomu za kuwani kuteuliwa kugombea ubunge kupitia vyama mbalimbali likiendelea, Chama cha Mapiduzi kimeonekana kutia fora zaidi ambapo hadi asubuhi Julai 16, 2020, zaidi ya wanachama 8,000 wametia nia.

Akizungumza hilo Rais Magufuli ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho amesema kuwa idadi hiyo inajumuisha wale wote waliochukua fomu za kuomba kugombea ubunge katika majimbo, viti maalumu pamoja na uwakilishi.

Akitaja idadi ya watia nia kulingana na mikoa amesema kuwa Mkoa wa Dar es Salaam unaongoza kwa kuwa na watia nia wengi zaidi ambapo hadi leo asubuhi walikuwa wamefikia 829, huku bado kukiwa na muda wa watu zaidi kuchukua fomu kabla ya muda wa mwisho ambao ni Julai 17.

Katika mikoa mingine Arusha wapo 320, Kusini Ungaji wapo 53, Kilimanjaro 82, Kagera wapo 328,.

Watia nia kwenye majimbo kupitia CCM ni 6,533 na kupitia viti maalumu ni 1,539 na kupitia wawakilishi ni 133, na hivyo kufanya jumla ya watia nia wote kuwa 8,205.

Rais Magufuli amesema kitendo hicho kinaonesha kuwa watu wanakipenda Chama cha Mapinduzi na pia ni ushahidi wa kuimarika kwa demokrasia ndani chama.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amekanusha taarifa zinazodai kuwa amewatuma baadhi ya watu kwenda kugombea, huku akikitaka chama hicho kuwapima watia nia wote kwa usawa kwa sababu hakuna aliyetumwa na kiongozi yeyote.

“Sijatuma mtu [kugombea ubunge]. Siwezi nikatuma mtu kupitia mgongo wa pembeni. Kama ningekuwa na uwezo wa kukutuma, kwanini nihangaike kukutuma, si ningesubiri tu kwenye viti vyangu 10 nikakuteua kama ningeshinda,” amesisitiza Rais.

Send this to a friend