Idadi ya wawekezaji nchi yazidi kupaa

0
42

Ziara za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye mataifa mbalimbali duniani zimezaa matunda kwa kufanya idadi ya wawekezaji nchini kuongozeka.

Rais Samia amekua akiwahakikishia wawekezaji kutoka nje kuja nchini kwani kuna mazingira mazuri ya uwekezaji na pia malighafi zote zinatohitajika katika shughuli za uwekezaji.

“Ndugu zangu mabibi na mabwana, serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi na rafiki kwa ufanyaji wa biashara na uwekezaji. Tunafahamu bila mchango wa sekta binafsi hatuwezi kuleta mageuzi makubwa ya uchumi wa nchi yetu.” – Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.

Pia, Rais Samia ameshawishi wawekezaji wengi kuja kuwekeza nchini kupitia filamu ya Royal Tour Tanzania ambapo ndani yake Mkuu huyu wa nchi ameonyesha vivutio vingi vinavyopatikana Tanzania hivyo kuzidi kuvutia wageni kuja kuwekeza nchi kwenye sekta ya utalii.

Hivi sasa, takwimu zinaonyesha kwamba idadi ya watalii wanaoingia nchini hususani jijini Dar es Salaam imeongezeka kwa asilimia 280 na Arusha asilimia 340 na hii ni kutokana na namna Rais Samia Suluhu anavyojitahidi kunadi utalii na vivutio vilivyopo nchini.

Tayari wawekezaji wameanza kuja nchini na kuwekeza kwenye maeneo mbalimbali huku Rais Samia alihamasisha kuonyesha ushirikiano kwao pindi wanapoonyesha nia ya kuja kuwekeza kwani kupitia wao ajira zitazalishwa na pia kubadilishana ujuzi wa mambo mbalimbali.

Baada ya kumalizikina kwa maonyesho ya sabasaba mwaka huu 2022, ilisainiwa mikataba 19 na wawekezaji waliotembela maonyesho hayo kutoka mataifa mbalimbali.

Mikataba 10 ya ujenzi wa viwanda vikubwa 500 vya kuchakata nafaka, kuuza na kununua mazao, ufugaji samaki, usafirishaji bidhaa kimataifa utakaokamilika mwaka 2025.

Mikataba 9 ya uwekezaji wa eneo maalum la viwanda la Sino Tan Park ambavyo ni Kwara vilivyopo Kibaha mkoani Pwani.

Viwanda hivyo vitazalisha ajira 500,000 ambapo 100,000 ajira za moja kwa moja na 400,000 za muda.

Send this to a friend