Idris Sultan ashtakiwa kwa kutumia laini ya simu ya mtu mwingine

0
73

Mchekeshaji kutoka nchini Tanzania, Idris Sultan amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam tayari kusomewa mashtaka yanayomkabili.

Sultan na mwenzake Innocent Maiga wamesomewa mashtaka mawili ambayo wamekana kuyatenda.

Katika shtaka la kwanza, Sultan anatuhumiwa kutumia laini ya simu iliyosajiliwa kwa jina la mtu mwingine, Innocent Maiga.

Shtaka la pili, Innocent Maiga anatuhumiwa kutoripoti mabadiliko ya umeiliki wa laini hiyo.

Watuhumiwa wote wamechaiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili, waliosaini bondi ya TZS 15 milioni kila mmoja.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 9, 2020.

Send this to a friend