Kwa mujibu wa tafiti, inakadiriwa kuwa kila mwaka mbwa wasiopungua milioni 10 na paka milio 4 wanachinjwa na kuuzwa kwenye soko la China peke yake.
Taifa hilo kubwa la Mashariki ya Mbali halina sheria ya kuwalinda wanayama hao, hali inayopelekea kuibwa kwa wingi wanyama hao na kuchinjwa kutokana na nyama hiyo kupendwa na kuliwa kwa wingi.
Wafanyabiashara wa mbwa na paka wanaponunuliwa au kuibwa katika maeneo tofauti husafirishwa na kwenda kuchinjwa kisha nyama yao kuuzwa kwenye mabucha au sokoni.
Katika nchi hiyo ulaji wa mbwa na paka umekithiri zaidi katika maeneo ya kusini, kati na Kaskazini Mashariki.