Ifahamu mikoa inayoongoza Tanzania kwa kutoa chanjo ya UVIKO19

0
44

Ikiwa ni zaidi ya miwili tangu kuzinduliwa kwa chanjo dhidi ya Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO19) nchini Tanzania, zaidi ya Watanzania 500,000 tayari wamepata chanjo hiyo.

Takwimu hizo zimetolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Morogoro ikiwa ni utaratibu wake wa kila wiki wa kutoa taarifa juu ya mwenendo wa utendaji wa serikali.

“Watanzania waliopata chanjo mpaka jana [Oktoba 1, 2021) ni zaidi ya 510,000 ambao wamepata chanjo, na zoezi la utoaji wa chanjo linaendelea,” amesema Msigwa.

Ameongeza kwamba ipo mikoa ambayo inafanya vizuri zaidi katika utoaji wa chanjo ambayo ni Katavi, Lindi na Mtwara.

Msigwa amesema ipo mikoa ambayo inazorota katika utoaji wa chanjo ukiwemo mkoa wa Morogoro, huku akiwataka wananchi kujitokeza na kupata chanjo kudhibiti athari kubwa za ugonjwa huo.

Ameeleza kuwa dozi 1,065,000 za chanjo ya Sinopharm kutoka China zinatarajiwa kuwasili nchini kuanzia Oktoba 4 mwaka huu, na amewataka wananchi ambao ni waoga wa sindano kuchangamkia chanjo ya Jansen inayochomwa mara moja, kwani Sinopharm itachomwa mara mbili.

Chanjo dhidi ya UVIKO19 ilizunduliwa nchini Julai 28 mwaka huu.

Send this to a friend