IGP Sirro: Wanasiasa acheni kuhamasisha uvunjifu wa amani Loliondo

0
45

Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro amesema zoezi la uwekaji alama kwenye Pori Tengefu la Loliondo wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha linakwenda vizuri na kuwataka wanasiasa kuacha kuwahamasisha wananchi wanaoishi kwenye maeneo hayo kuleta uvunjifu wa amani.
 
Amesema hayo leo Juni 13 wakati alipofika katika tarafa ya Loliondo kuonana na  askari waliopo katika operesheni ya uwekaji mipaka katika pori hilo.
 
Aidha, amesema kufanyika kwa zoezi hilo ni kwa ajili ya manufaa ya watanzania na kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
 
Naye Mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongella amesema ujio wa Mkuu wa Jeshi la Polisi kwenye eneo hilo umesaidia kujenga hamasa na morali kwa askari walioko katika operesheni hiyo.

Send this to a friend