IGP Wambura afanya mabadiliko Makamanda wa Polisi

0
63

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura amemhamisha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, (SACP) Ulrich Matei kwenda Makao makuu ya Polisi Dodoma.

Awali Kamanda Matei alikuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, na nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara Kamishna Msaidizi wa Polisi, (ACP) Benjamini Kuzaga.

Madaktari waomba wanaojaribu kujiua wasishtakiwe

Aidha, IGP Wambura amemhamisha Kamishna Msaidizi wa Polisi, (ACP) George Katabazi kutoka Makao makuu ya Upelelezi Dodoma kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara .

Kamanda Katabazi anachukua kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi, (ACP) Benjamini Kuzaga aliyehamishiwa kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya.

Taarifa imeeleza kuwa mabadiliko hayo ambayo yalianza Septemba 08, 2022 ni katika kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa majukumu ya Jeshi la Polisi.

Send this to a friend