Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura amemhamisha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Fortunatus Muslim kwenda Kitengo cha Mipango Makao Makuu ya Polisi Dodoma.
Nafasi ya Kamanda Muslim inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Alex Mukama ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe.
Rais Samia ateua wapya sita, yumo David Kafulila
Katika mabadiliko hayo, IGP Wambura amemhamisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Theopista Mallya kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe.
Aidha, amemhamisha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Shedrack Masija ambaye alikuwa Afisa Mnadhimu Namba Moja Mkoa wa Simiyu kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa.