IGP Wambura afanya uhamisho wa makamanda wa mikoa

0
74

Mkuu wa Jeshi la Polisi, Camillus Wambura amewahamisha mikoa ya kazi baadhi ya makamanda wa Polisi na mmoja kumhamishia Makao Makuu ya Polisi Jjjini Dodoma.

Waliohamishwa ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Henry Mwaibambe ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, amehamishiwa mkoani Tanga kuwa Kamanda wa Polisi mkoani humo.

Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Safia Shomary amehamishiwa Mkoa wa Geita kuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo.

Pia aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temke, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Richard Ngole amehamishiwa Mako Makuu ya Polisi Dodoma na nafasi yake imechukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Kungu Malulu ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji.