IGP Wambura awahamisha baadhi ya Makamanda wa Polisi

0
74

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Camillus Wambura amempangia Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ulrich Matei kuwa Mkuu wa Kitengo cha Polisi Wasaidizi na Kampuni Binafsi za Ulinzi nchini  ambapo anachukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Issaack Katamiti.

Aidha, amemhamisha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, (SACP) Ramadhani Ng’anzi ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza na kwenda kuwa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania.

Awali, aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, (SACP) Wilbroad Mtafungwa anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza.

Naye, aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Protus Mutayoba amekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rufiji baada ya Kamanda wa Mkoa huo kuhamishiwa Mkoa wa Kipolisi Temeke.