IGP Wambura: Hali ya usalama nchini ni shwari

0
83

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura amesema hali ya usalama nchini ni shwari kutokana na kazi nzuri inayofanywa na Jeshi la Polisi ambapo amevipongeza vyombo vya ulizi na usalama kwa kuhakikisha nchi inakuwa na amani na utulivu na wananchi wanaendelea na shughuli zao.

Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Mkutano mkuu wa Mwaka wa Maafisa wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro ambapo mgeni rasmi wa mkutano huo alikuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Daniel Sillo.

Aidha, IGP. Wambura amesema jeshi la polisi limejiimarisha zaidi katika mikakati ya kuzuia uhalifu ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza wakati wa kuwashughulikia waalifu, na kutoa rai kwa viongozi wa dini na familia kulea jamii kwa kufuata mila, desturi na misingi ya dini.

Mbali na hayo, IGP. Wambura amesema katika kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025, Jeshi la polisi limejipanga vyema kuimarisha usalama kwenye chaguzi hizo na kuwaomba wananchi kutokuwa na wasiwasi.

Send this to a friend