Imam miaka mitano jela kwa kuua Nguruwe Msikitini

0
46

Mahakama moja Mashariki mwa Rwanda imemhukumu Imam wa msikiti, Sadate Musengimana kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la kuua nguruwe msikitini.

Imam amekiri kumuua nguruwe huyo na kudai kuwa ‘ilikuwa bahati mbaya’ wakati nguruwe alipofika karibu na msikiti na kuvuruga mafundisho yake ya quran Februari mwaka huu.

Hata hivyo mashahidi waliiambia mahakama kuwa walimwona Musengimana akimpiga kwa nguvu nguruwe huyo kwa kipande cha mbao na kumuua papo hapo, na wengine kudai kuwa hakuwa na nia ya kumuua.

Awali upande wa mashtaka uliomba kifungo cha miaka saba jela dhidi ya mtuhumiwa huku wakili wa Musengimana akilaani hukumu hiyo kwa madai kuwa mteja wake alimuua mnyama huyo kwa bahati mbaya.

Awali upande wa mashtaka uliomba kifungo cha miaka saba jela dhidi ya mtuhumiwa huku wakili wa Musengimana akilaani hukumu hiyo kwa madai kuwa mteja wake alimuua mnyama huyo kwa bahati mbaya.

Send this to a friend