IMF: Afrika lazima ifanye mambo haya matatu kujikwamua kiuchumi

0
22

Mkutano wa kila mwaka wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia uliopangwa kufanyika huko Marrakech, Morocco Oktoba mwaka huu, unatarajiwa kuleta suluhu juu ya mambo mbalimbali yanayohusu bara la Afrika na pia ni mkutano wa kipekee kwani itakuwa mara ya kwanza katika miaka 50 kufanyika Afrika.

Kristalina Georgieva, Mkurugenzi Mkuu wa IMF ameeleza kwamba ili bara la Afrika liweze kukuza uchumi wake linahitaji kufanyia kazi katika maeneo matatu, mojawapo ni kuimarisha ushirikiano baina ya nchi katika kujenga miundombinu bora ya usafiri na mawasiliano ili kuwezesha biashara na ushirikiano, pili, kuondoa vizuizi vya biashara na visivyo vya biashara.

“Tumefanya utafiti kuhusu jinsi mkataba wa biashara huria wa bara unavyoweza kuleta manufaa kwa Afrika ikiwa vizuizi vya biashara na visivyo vya biashara vitataolewa, biashara ndani ya Afrika inaweza kuongezeka kwa asilimia 53, biashara kati ya Afrika na sehemu nyingine za dunia kwa asilimia 15, na kipato halisi kwa kila mtu kinaweza kukua kwa asilimia 10,” ameeleza.

Rais Kagame aonya shughuli za kidini zinazotukuza umasikini

Eneo la tatu alilotaja ni kuanzisha mifumo ya kifedha ya kidijitali ili kuwezesha biashara na shughuli za kifedha kwa njia ya kidijitali itakayosaidia kuongeza ufanisi na kusaidia ukuaji wa biashara.

Kiongozi huyo amesema ana matumani kuwa bara la Afrika linaweza kufanikisha kujiinua kiuchumi kwa kiwango kibwa kutokana na uongozi wake imara pamoja na watu wake.

“Kuna harakati na pia kuna maendeleo katika muktadha wa kikanda. Kwa maneno mengine, bara hilo pia lina mikataba yake ya kikanda na huko tunashuhudia harakati zaidi ambapo kuna uongozi imara. Pale ambapo kuna nia, kuna njia.

Kwanini ninamatumaini kuhusu Afrika? Ni bara la kushangaza, lenye watu wenye akili na nguvu. Hawa ndio watakaounda sana karne hii na nawatakia kila mafanikio kwenye bara hilo,” ameongeza.

Send this to a friend