IMF kuikopesha Tanzania trilioni 2.4

0
47

Bodi ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) imeridhia mkopo wa Dola za Marekani bilioni 1.046 (sawa na zaidi ya TZS trilioni 2.4) kwa Tanzania katika kipindi cha miezi 40 kusaidia kukabiliana na athari za vita ya Urusi na Ukraine.

Taarifa ya IMF inaeleza kuwa vita hiyo inakwamisha uchumi wa Tanzania kuimarika kufuatia mlipuko wa UVIKO-19, hivyo kuleta changamoto zaidi katika maendeleo.

Tanzania ilipokea mkopo wa dola milioni 567 mwishoni mwa 2021 ili kukidhi mahitaji yake ya dharura wakati mlipuko huo ulipoathiri maendeleo ya kiuchumi, hususan sekta ya utalii kwa kiasi kikubwa.

Katika kiasi hicho cha mkopo kitakachotolewa, dola za Marekani milioni 151.7 zitatolewa mara moja.

Send this to a friend