Umoja wa mataifa (UN) umetoa ripoti kuwa idadi ya watu duniani itafikia bilioni nane ifikapo Novemba 15 huku India ikitarajiwa kuchukua nafasi ya China kama taifa lenye watu wengi zaidi duniani.
Ripoti hiyo imetolewa katika siku ya kimataifa ya idadi ya watu duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka 11 Julai 11.
Rais wa Sri Lanka akimbia nchi
Umoja wa Mataifa umesema, kuna uwezekano kuwa idadi ya watu ulimwenguni ikafikia bilioni 8.5 ifikapo mwaka 2030, bilioni 9.7 kwa mwaka 2050 na kufikia bilioni 10.4 ifikapo mwaka 2080.
Kaulimbiu ya mwaka huu ni ‘ulimwengu wa bilioni 8 kuelekea mustakabali thabiti kwa wote, kutumia fursa na kuhakikisha haki na maamuzi binafsi kwa wote.’