
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza mabadiliko ya takwimu za idadi ya wapigakura, ambapo jumla ya wapigakura waliopo katika Daftari la Kudumu la Wapigakura ni 37,647,235 badala ya 37,655,559 iliyotangazwa awali.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi INEC, Ramadhani Kailima imesema idadi hiyo ya wapigakura ni sawa na ongezeko la asilimia 26.53 kutoka idadi ya wapigakura 29,754,699 waliokuwa kwenyw Daftari la Wapigakura mwaka 2020.
“Kati ya wapigakura 37,647,235, wapigakura 36,650,932 wapo Tanzania Bara na Wapigakura 996,303 wapo Zanzibar,” imesema.
Aidha, INEC imetangaza pia kuwa vituo vya kupigia kura vitakuwa 99,895; Tanzania Bara vikiwa 97,348 na Zanzibar vikiwa 2,547. Hiyo ni baada ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar kufanya marekebisho ya vituo.






